WATOTO WA KIZUNGU WAIPA UNDER THE SAME SUN ZAIDI YA MILIONI MOJA ZA KITANZANIA

 by maasinda blog

Watoto wanaosoma shule ya vipaji ya Internation School of Tanganyika wakiwa kwenye picha ya pamoja na  wadau kutoka shirika la kutetea watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) la Under The Same Sun, baada ya mkutano wao na waandishi wa habari kufanyika leo katika Makao makuu ya Shirika hilo.

Katika Mkutano huo, watoto hao wametoa msaada wa zaidi ya Shilingi Milioni Moja za Kitanzania pamoja na Mafuta ya kuzuia Makali ya Jua kwa walemavu wa ngozi, ambapo wamepata pesa hizo baada ya kuuza vitabu walivyoviandika wenyewe wakiwa shule pamoja na kuuza Fulana walizozitengeneza wenyewe wakiwa Shuleni hapo. Watoto hao kutoka nchi mbalimbali wamesema kuwa Vitabu na fulana zao, nyingi wameziuza nchini   Zanzibar.

Watoto hao pia walifanikiwa kupiga picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi  Vicky Ntetema ,  na wanaonekana wakiwa katika nyuso za furaha kabisa. Ambapo Bi Nketema amewataka Watanzania kuwa na Mtizamo Chanya wa kuwasaidia Albino kwa kuiga Mfano wa watoto hao
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: