WANA BUSEGA DAR ES SALAAM WAPEWA WITO NA MWENYEKITI WAO

Mkt wa (BIDECO) Bw Joseph Ginhu
    Wakazi wanaotoka  kanda ya ziwa hususani wale wanaotoka Simiyu katika wilaya ya Busega   ambao wanaishi jijini Dar es salaam wametoa wito kwa viongozi na wanasiasa wanaotoka katika wilaya hiyo kutokuingiza siasa katika maswala ya maendeleo na badala yake kukaa kwa pamoja na kujadili njia za kuinua wilaya hiyo katika maswala ya maendeleo.
        Hayo yamesemwa na mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wana busega  (BUDECO)  Bw JOSEPH GINHU katika mkutano mkuu wa jumuiya hiyo ambayo ni mkusanyiko wa wakazi wanaotoka katika wilaya ya busega mwanza  waliopo jijini dare s salaam wenye lengo la kuinua wilaya hiyo kimaendeleo
        Bw JOSEPH amesema ni kawaida katika jumuiya kama hizo zenye lengo la kutafuta maendeleo ya mahali Fulani kutokea watu wanaotafuta maslahi yao kwa kuingiza siasa jambo ambalo amelikemea na kusema katika jumuiya yao hawataliruhusu litokee.
        Aidha amesema lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni baada ya kugundua wilaya ya busega inayopatiakana mwanza imesahaulika kimaendeleo kitu ambacho kimewasukuma kuanzisha umoja huo ili kuiletea maendeleo wilaya yao.
        Hata hivyo Bw JOSEPH ametoa wito kwa wakazi wanaotoka katika wilaya hiyo kujiunga na jumuiya hiyo ili kuisaidia wilaya ya busega  huku akisema hadi sasa wamefanikiwa kupata wanachama 107 .
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: