MSANII WA BONGO MUVI ADAIWA KUMTELEKEZA MTOTO NA MKE KIJIJINI KWAO KAHAMA NA KUZAMIA DAR

;

MSANII MWENYEWE HUYU HAPA

TUNDA MTOTO ANAYEDAIWA KUTELEKEZWA NA BWANA TONY

TUNDA MTOTO ANAYEDAIWA KUTELEKEZWA NA BWANA TONY

SOMA ALIVYONIELEZEA SAKINA WA KAHAMA

habari naitwa sakina mimi ni mtangazaji wa radio hapa kahama. kuna habari nyingi ninazozipata huku nimeona nianze na hii…

huyu jamaa ambae nimeambatanisha picha zake ni msanii ambae anajiona maarufu anaetokea hukuhuku kahama ila kwa sasa yuko dar. anafanya kzi yake ya sanaa kwenye kampuni ya tuesday film entaiteinment.  jamaa huyu ambae amewahi kucheza filamu ya ”BEAUTIFUL” kama mpenzi wake ray c aliyekuwa anaishi porini na ambae anajulikana sana kwa jina la ‘TONY WA RAY C’ anadaiwa kutelekeza mtoto wa kike wa miaka sita kwa maelezo yafuatayo…

juzi asubuhi alikuja dada mmoja hapa ofisini kwetu nikamkaribisha na akaanza kunielezea kwamba ye anaitwa ‘JUSTINA IKOMBE’  alikuwa mchumba wa msanii huyo ambae jina lake kamili ni ‘JANUARY NYANDA’ , na hata wakafikia kuzaa nae mtoto mmoja wa kike anaejulikana kwa jina la ‘TUNDA’  lakini baada ya dada huyu kujifungua jamaa huyo aliaga anakwenda dar. kufanya shughuri zake za sanaa na tangu hapo hana mawasiliano nae wala hajui binti huyu anaishije na mtoto. na mbaya zaidi ni kwamba mama wa mtoto anapojitahidi kumtafuta jamaa humkatia simu akionyesha kutokuwa na shida kabisa ya kuongea nae na mpaka hivi sasa mtoto amekua na anahitaji kwenda shule lakini hakuna msaada wowote…binti huyo alikuwa akiongea kwa uchungu kiasi cha kunihuzunisha hata mimi pia kama mwanamke mwenzake…nilimuomba namba za msanii huyo ambazo ni 0756 570907 na nilipopiga na kujitamburisha jamaa alinijibu matusi kama hana wazazi akidai kuwa hamfahamu huyo binti na wala yeye hana mtoto anaeishi kahama na wala yeye mwenyewe hajawahi kuishi kahama, na wakati amezaliwa kahama katika kijiji kinachoitwa ‘kagongwa’ na amesoma shule ya msingi ‘KISHIMA’  na secondary ‘ISAGEHE’ na mpaka sasa wazazi wake wote wanaishi hapa kijijini ‘kagongwa’
baada ya majibu hayo sikuwa na cha kuongea zaidi ya kuomba picha za msanii huyo pamoja na za mwanae huyo na kumuahidi dada huyo kwamba hili swala sitolifumbia macho, nitalitangaza kwenye vyombo vya habari kadri ya uwezo wangu na iwe fundisho kwa watu maarufu wengine wenye tabia kama za jamaa huyu…
naomba tushirikiane kuwatetea wanawake… ahsante
                                                         by.    dj sakky         ”the true girl”

NAOMBA KUWASILISHA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: