SOMA ALICHOKISEMA KIBANDA KUHUSU WALIOMVAMIA

Akizungumza kwa tabu alipokuwa chumba cha wagonjwa ICU, Hospitalini Moi, alisema, “Nilifika nyumbani kwangu kama saa 6 usiku nikitokea kazini tulikuwa tunafuatilia uchaguzi wa Kenya tukaona hamna la maana.

Nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu… Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kukimbia kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito… niliona kama watu 3 hivi…

Sikufahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande ‘mshuti…mshuti’ huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu kushuti’ ilikuwa kama vile imegoma.

Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaningoa meno na kucha ktk vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi pembeni ya nyumba na kunitupa na wakaondoka, badaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.

HABARI KWA HISANI YA JAMII FORUM

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: