SOMA ALICHOKISEMA DIAMOND JUU YA TUKUMA ZINAZOMKABILI

     MSANII anayeaminika kuwa na nyota ya kupendwa na mashabiki na wadau wengi wa muziki wa kizazi kipya hasa wanawake, Naseeb Abdul au Diamond Platinumz kama anavyojiita,  amejitokeza kujibu tuhuma kadhaa zinazomkabili.

          Hatua hiyo imekuja baada ya maswali mengi kuibuka na shutuma nyingi kumwangukia kupitia vyombo mbalimbali vya habari, huku akiwa amekaa kimya, kiasi cha kufanya baadhi ya watu kutoelewa ni kwa nini ameamua kutozungumza chochote.

               Moja ya tuhuma kubwa inayomkabili ni kuhusiana na mganga wa kienyeji anayehangaika kwenye vyombo vya habari na kudai kwamba amemfikisha Diamond hapo alipo lakini kwa sasa amekimbiwa na msanii huyo.

             Akijibu tuhuma hiyo akasema kwamba kwanza hamjui huyo mganga, ila kiukweli ni kwamba  kuna watu wanataka kumchafua, na kama ni mganga kweli na kakimbiwa na mteja aliyempandisha kwa nini asitumie uganga kumshusha?

           “Mganga wa kweli jamani hawezi kukimbilia kwenye vyombo vya habari, mganga wa kweli anamalizana na mteja kimya kimya na mteja mwenyewe anajikuta anarudi kwa mganga kuomba radhi, huyu sio mganga, ingawa simjui!”

             Tuhuma ya pili ni kuhusiana na maonyesho yake kudorora ambapo pia mganga huyo amehusishwa, kwamba yeye ndiye aliyemlaani na kusababisha mambo ya mwanamuziki huyo anayefikiriwa kuwa ni tajiri kuliko wenzake, kuanza kwenda mrama.

           Jibu alilolitoa ni kwamba hakuna jambo lake hata moja linalokwenda vibaya. Picha zilizochapishwa na gazeti moja la kila wiki, likionyesha ukumbi ukiwa mtupu katika onyesho ambalo alilifanya Arusha, zilipigwa mwanzoni, wakati hapakuwa na mashabiki wengi waliokuwa wameingia, ukumbi baadaye ulijaa.

              “Na kama ni maonyesho, nina ratiba ya show mpaka mwezi wa saba, sasa nimeshuka vipi jamani?”, alisema huku akionekana mwenye masikitiko makubwa kwa kile anachosema anaonewa tu na maneno hayo ya uzushi.

           Habari nyingine kubwa iliyoenea mjini ni ile inayohusiana na uhusiano wake na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Entertainment Masters, Peniel Mungilwa ambapo katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakionekana mara kwa mara wakiweka picha zao zinazoonyesha dhahiri wapo katika mapenzi.

              Hili alionekana kama kushtushwa nalo ingawa baadaye alijiweka sawa na kusema ni sinema tu za hapa na pale lakini si ukweli kwamba wana uhusiano.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: