WALIMU WAPYA WAANZA KUCHEKELEA AJIRA

BREAKING NEWZZZ

 

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mh dkt SHUKURU KAWAMBWA ametangaza rasmi kutoka kwa ajira  za waalimu wapya wa shule za msingi,secondary na vyuo vya ualimu Tanzania bara kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013.

 

Akitangaza nafasi hizo KAWAMBWA amesema, jumla ya walimu 26,527 wameajiriwa serikalini kwa mwaka huu, huku ikiwa ni pamoja na walimu 13,526 waliopangwa kufanya kazi kwenye shule za msingi zilizopo kwenye halmashauri,na waalimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za mazoezi zilizo chini ya wizara ya elimu,huku akiongeza kuwa jumla ya walimu wa sekondari na vyuo vya ualimu walioajiriwa ni 12,973 wakiwemo wa shahada na stashahada.

 

Waziri KAWAMBWA amesema kutokana na tatizo la kutokuwa na walimu wa kutosha  katika maeneo ya vijijini wizara katika ajira hizo imetoa kipaumbele katika maeneo hayo ya vijijini kwa kupeleka walimu wengi tofauti na mijini.amesema ajira kwa walimu kwa mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 11 tofauti na ilivyokuwa mwaka jana.

 

Hata hivyo amesema kuwa tarehe rasmi za walimu kuripoti katika vituo vyao vya kazi ni kuanzia tarehe 1 march hadi kufikia tarehe 9 march mwaka wa 2013,huku akisema ni muda wa kutosha kwa walimu wote kuripoti katika vituo vyao vya kazi

 

Aidha ameongeza kuwa baada ya tarehe hizo za kuripoti kupita serikali haitamvumilia mwalimu yoyote ambaye atakuwa hajaripoti kazini na badala yake atakuwa amejiondoa kwenye ajira hiyo yeye mwenyewe,huku akiwaondoa hofu walimu kuhusu mazingira ya kufanyia kazi kwa kusema serikali itahakikisha inaboresha maslahi kwa walimu ili waweze kufanya kazi kwa kujituma.

 

 

Advertisements

1 Comment

  1. elias msechu said,

    February 13, 2013 at 12:36 pm

    sana 2


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: