VURUGU ZANZIBARI CUF YATOA YA MOYONI

 

Chama cha Wananchi CUF kinasikitishwa na matukio ambayo hayakutarajiwa kutokea hapa Zanzibar yaliyoanza kujitokeza jana tarehe 17/10/2012 ambayo yamesababisha vurugu kubwa katika Manispaa ya Zanzibar na vitongoji vyake.

Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa Maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto maskani za CCM. Matukio mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha kufuatia vurugu hizo ni kuwepo taarifa za kuuwawa kwa Askari Polisi.

Kutokana na vitendo hivyo, Chama Cha wananchi CUF kinaalaani kwa nguvu zote matukio hayo ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na kusababisha hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.

Sambamba na vurugu hizo, Chama Cha Wananchi CUF kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyotolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed iliyoeleza juu ya kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha.

Katika Taarifa hiyo, Serikali imethibitisha kuwa vyombo vyake vyote vya ulinzi havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu na wasi wasi kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi huyo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.

Chama cha Wananchi CUF kinaiomba Serikali kuendeleza juhudi zote za kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na Serikali hii ni kwajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi wasi ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.

Aidha, Chama cha wananchi CUF kinawataka wanachama wake, wapenzi na wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi yetu.

Sote kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta vurugu kwa vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi hii ya Zanzibar ambayo imejijengea duniani kote.

Haki sawa kwa Wote

………………………..
Salim Biman
Kaimu Naibu katibu Mkuu Zanzibar

  NA MWANISHI WAKO EXAUD MTEI KWA USHIRIKIANO NA JAMII FORUM
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: