RIPOTI YA TUKIO LA MTOTO KUKOJOLEA KURUAN HII HAPA

 

Baada ya mtoto mwenye miaka 13 huko mbagala kufanya kitendo ambacho kimewaacha watu na jazba kubwa hususani waislam cha kukojolea kitabu kitakatifu cha waislaam wakati akibishana na mwenzake leo mchana ,Mkuu wa mkoa wa dar es saam SAID MECK SADIKI  na kamanda wa polisi mloa wa dare es salaam wamezungumza na watanzania kupitia television ya taifa kuelezea kilichotokea

  kamanda wa polisi suleman kova amesema kilichotokea ni mabishano ya watoto hao wakibishana kuwa ukikojolea kitabu hicho utapata madhara ndipo mtoto huyo alipoamua kufanya hivyo ili kuona kama ni kweli,kamanda kova amesema baada ya mtoto huyo kufanya hivyo mwenzake alienda kuripoti kitendo hicho msikitini ndipo matatizo yalipoanzia.

   amesema baada ya report za tukio hilo kufika msikitini watu walianza kumtafuta mtoto huyo ili kumwadabisha ndipo polisi walipoanza kazi yake mna kumchukua mtoto huyo na kumweka ndani.

  Ameendelea kusema baada ya hapo ndipo wananchi walianza kukizingira kituo cha polisi ili kumtoa mtoto huyo na kumpa adhabu.baada ya hali kuwa mbaya ndipo polisi waliamua kuwatawanya wananchi kwa mabom.

Kova amesema kitendo hicho kisihusishwe na uhasama wa kidini kwani aliyekifanya kitendo hicho ni mtoto mdogo saana na hakujua madhara yake na anajuta kufanya hivyo.pia kamanda amedhibitisha kuvamiwa kwa makanisa matatu na kuharibiwa vibaya na wananchi hao.

naye mkuu wa mkoa amewaomba watanzania kulipuuzia tiukio hilo kwani aliyelifanya ni mtoto na hakujua madhara yake,hata ivyo hali katika maeneo hayo ya mbagala imerejea katika usalama kama kawaida

    

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: