Makada 201 CCM wahamia CHADEMA

MAKADA 201 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mwenyikiti wa Kitongoji cha Buhungu, Kata ya Kigongo, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kujiunga CHADEMA kwa wana CCM hao kunatokana na mikutano ya vuguvugu la mabadiliko (M4C), inayofanywa na chama hicho cha upinzani katika************* maeneo mbalimbali likiwemo Jimbo la Chato, ambalo Waziri wa Ujenzi, John Magufuli ndiye mbunge wake.
Makada waliotimkia CHADEMA kwa nyakati tofauti ni kutoka Kijiji cha Muganza, Kasenga, Busaka na Igando, Kata ya Bwera ambapo walidai kuchoshwa na mwenendo wa siasa za CCM, hali ambayo imewasababisha waendelee kuwa na maisha magumu huku viongozi wao wakiendelea kuneemeka.
Mbali ya makada hao wengine waliojiunga na CHADEMA ni Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM kata ya Muganza Paulo Malulu, Katibu wa Tawi la CCM Kijiji cha Mkombozi, Christopher Charles na Mwenyekiti wa kitongoji cha Buhungu Kata ya Kigongo, Razaro Busumabu.
Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo, kwenye Kata ya Muganza, Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Chato, Alex Mukama, alisema wananchi wa Jimbo la Chato wamekipokea chama hicho tofauti na awali waliogopa kujitokeza hadharani.
Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Ludomya, aliwataka wananchi kukipa kisogo CCM kwa kuwa kimeshindwa kuboresha maisha ya wananchi kwa miaka yote.

SOURCE:
TANZANI DAIMA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: