FBI WAFIKA ARUSHA KUCHUNGUZA TUKIO LA KIGAIDI LA KANISA KUPIGWA BOMU

MAJASUSI wa shirikisho la ujasusi la nchini Marekani wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini Tanzania katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa Vatican nchini siku ya jumapili.
 
Magesa alitoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipozuru eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali na kuwapa pole.
 
Wakati maafisa hao wakifika jijini humo tayari vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao wakiwemo watu wanne kutoka Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja kabla ya tukio.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa watu hao walikamatwa muda mfupi wakiondoka nchini kupitia mpaka wa Namanga kuelekea nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
 
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi zitatolewa kadri muda na wakati utakavyoruhusu.
Advertisements

BAADA YA RUGE KUFUNGUKA JUU YA KAULI YA LAD JAY DEE, MWANADADA HUYO NAYE KASEMA YA MWANZO ILIKUWA TREILA 2.

 
          Hakuna tatizo kwa redio kutopiga nyimbo ya msanii yoyote kwan redio hujiendesha yenyewe. Magic Fm imekaa mdaa mrefu bila kupiga nyimbo za diamond na hata east Africa redio ilikaa mdaa mrefu bila kupiga nyimbo ya ray c, amesema ruge mutahaba
  
      Akizungumza leo asubuhi katka kipindi cha power breakfast  Mkurugenzi wa Clouds Entertainment RugeMutahaba amezungumzia suala ambalo limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na midomoni mwa watu kuhusiana na LADY JAY DEE kutoa kashfa nzito.
 
RugeMutahaba
        Ruge amesema nchi kama nchi tunatakiwakujadili mambo ya msingi na siyo binafsi na kuwa kimya muda mrefu kutoongelea  tatizo hili kwasababu halina maslaiya taifa inatakiwa tukae tumalize binafsi na hajui tatizo ni nini .
 
         Clouds fm ni chombo binafsi iliyosajiliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwa kufuata Masharti tofauti na kuchagua vitu vyao kuwa ni Redio ya burudani na inapanga wao nyimbo za kupiga na sio mtu mwingine na KUSEMA  WANAWEZA KUAMUA  WASIPIGE NYIMBO YEYOTE YA BONGO FLEVA.
 
     Pia Ruge amesema kila mtu mzuri akifanya kitu kizuri lazima kiwe na lawama na tatizo hili limeanza vipi yeye afahamu chochote .
 
      Amesema wana record ya kupiga wimbo mpya wa jay dee mara 46 kwa hiyo haelewi kwanin anasema hwapigi nyimbo zake.
 
      Ameongeza kuwa LADY JAY DEE  anahofia band ya sky right ambayo inamilikiwa na SEBASTIAN NDEGE ambaeni mfanyakazi wa mwandamizi wa CLOUDS MEDIA GROUP.
 
 
“Sky rights imeanza kwa kuchukua wanamuziki toka bendi mbalimbali ikiwemo ya lady jay dee lakin sio chanzo cha kuigopa. So jay dee anatakiwa apelike makombora yake kwa sky rights sio kwangu” amesema Ruge
 
 
    Aidha  Ruge amesema kuwa muziki ni mchezo wa kupokezana vijiti na mtu uwezi tawala sku zote kwani sasa kuna watu  wanakuja juu sana kama kina ommy dimpoz.
 
     Kuhusu Lina na barnaba kutopiga show amesema kuwa tatizo ni hawakupatana vizuri kwenye suala la malipo.
 
          Amesema kuwa clouds media group inafanya tamashamoja kwa mwaka kwa hiyo wanaosema kuwa wanawanyonya wasanii kwenye show wanatoa wapi ayo.
 
       Ameongeza kuwa clouds media group huwazamini wasanii kila week kupiga show kwenye kumbi za bilcanas na maisha club.
 
                                LAD JAY DEE NAYE KUPITIA PAGE YAKE YA FACEBOOK KASEMA HAYAA.
 
LADY JAYDEE
              Kama mtakumbuka niliahidi kutoa awamu ya pili tar 15 au 17 May na ahadi ni deni..Japo naona mbali ila Nitafanya hivyo, bado nina mengi sana ya kuzungumza kuhusu Ruge na wenzake…Ile ilikuwa ni trailer tu, Movie ndio linaanza sasa #TeamAnaconda no surrender.

MAJAMBAZI WAMVAMIA BINTI NA KUMUUA KISHA KUMPORA KIASI CHA TSH MILIONI 10

Majambazi yapora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi muda mchache uliopita na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 jioni inavyosemekana mdada huyo  alikua akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. Mpaka tunaingia mitamboni hakuna habari yoyote ya kukamatwa kwa wahalifu hao.na blog ya wananchi
 

TUKIO LA KULIPUKA KWA BOMU JANA ARUSHA HILI HAPA.

Kanisa katoliki parokia ya Olasiti ambalo leo hii lilikuwa linapandishwa hadhi ya kuwa Parokia lililolipuliwa na kitu kinachosemekana kuwa ni bomu mapema leo hii wakati ibada ikiendelea ambapo katika Ibada hiyo Balozi wa Papa alikuwa amehudhuria na ndiye aliyekuwa azindue Parokia hiyo.
Katika Sehemu iliyowekwa alama ya Pembe tatu ndipo kifaa hicho kinachosadikiwa kuwa ni bomu kilipo angukia na kulipuka na kujerui zaidi ya watu Ishirini ambapo inasidikika kuwa mtu mmoja amefariki Dunia.
Waumini walikuwa wamekaa eneo hili, ambapo baada ya Mlipuko huo eneo hilo lilizungushiwa uzio na Usalama  kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hawa ni Baadhi tu ya Majeruhi
Huyu Bwana naye ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi, alijeruhiwa na Kitu hicho
Watu walikimbia Ovyo ovyo bila kujali kuwa wamesahau viatu vyao.

MAASINDA BLOG INATOA POLE KWA WALIOFIKWA NA MATATIZO HAYO NA KUWATAKA WAKRISTO WOTE KWA UJUMLA, KULIWEKA SWALA HILI KATIKA MAOMBI PAMOJA NA KUOMBA AMANI KWA AJILI YA TAIFA LETU.

 

MAJAMBAZI WALIOUAWA NA POLISI MBEYA JANA HAWA HAPA

 

HABARI NA  MR SEMVUA MSANGI BLOG

 
Kamanda Diwani akionyesha silaha walizokuwa wakitumia majambazi hao.
 
Kamanda Diwani akiangalia gari lililokuwa likitumiwa na Majambazi hao
 
Hawa ndio majambazi Waliouawa
 
    GARI LA MAJAMBAZI HAO
 
ASKARI WAKIANGALIA SILAHA ZILIZOIWEKWA MEZANI ZILIZOKUWA ZIKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO
 
HAO KAMANDA OTHMANI AKISISITIZA JAMBO BAADA YA KUWATIA NGUVUNI MAJAMBAZI HAYO.
 
MOJA YA SILAHA KUBWA ILIYOKUWA IKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO IKIWA MEZANI
 
Kamanda diwani akionyesha wskari wenzie moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha
MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa  baada ya watu watano wanaodahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.
Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo  ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
Picha na Mbeya yetu

WANA BUSEGA DAR ES SALAAM WAPEWA WITO NA MWENYEKITI WAO

Mkt wa (BIDECO) Bw Joseph Ginhu
    Wakazi wanaotoka  kanda ya ziwa hususani wale wanaotoka Simiyu katika wilaya ya Busega   ambao wanaishi jijini Dar es salaam wametoa wito kwa viongozi na wanasiasa wanaotoka katika wilaya hiyo kutokuingiza siasa katika maswala ya maendeleo na badala yake kukaa kwa pamoja na kujadili njia za kuinua wilaya hiyo katika maswala ya maendeleo.
        Hayo yamesemwa na mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wana busega  (BUDECO)  Bw JOSEPH GINHU katika mkutano mkuu wa jumuiya hiyo ambayo ni mkusanyiko wa wakazi wanaotoka katika wilaya ya busega mwanza  waliopo jijini dare s salaam wenye lengo la kuinua wilaya hiyo kimaendeleo
        Bw JOSEPH amesema ni kawaida katika jumuiya kama hizo zenye lengo la kutafuta maendeleo ya mahali Fulani kutokea watu wanaotafuta maslahi yao kwa kuingiza siasa jambo ambalo amelikemea na kusema katika jumuiya yao hawataliruhusu litokee.
        Aidha amesema lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni baada ya kugundua wilaya ya busega inayopatiakana mwanza imesahaulika kimaendeleo kitu ambacho kimewasukuma kuanzisha umoja huo ili kuiletea maendeleo wilaya yao.
        Hata hivyo Bw JOSEPH ametoa wito kwa wakazi wanaotoka katika wilaya hiyo kujiunga na jumuiya hiyo ili kuisaidia wilaya ya busega  huku akisema hadi sasa wamefanikiwa kupata wanachama 107 .

CHEKA ALIVYOCHEKA JANA

Bondia Fransic Cheka Kushoto akipambani na Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi

Bondia Fransic Cheka Kushoto akimshambilia kwa makonde ya nguvu Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika katika sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi

WATOTO WA KIZUNGU WAIPA UNDER THE SAME SUN ZAIDI YA MILIONI MOJA ZA KITANZANIA

 by maasinda blog

Watoto wanaosoma shule ya vipaji ya Internation School of Tanganyika wakiwa kwenye picha ya pamoja na  wadau kutoka shirika la kutetea watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) la Under The Same Sun, baada ya mkutano wao na waandishi wa habari kufanyika leo katika Makao makuu ya Shirika hilo.

Katika Mkutano huo, watoto hao wametoa msaada wa zaidi ya Shilingi Milioni Moja za Kitanzania pamoja na Mafuta ya kuzuia Makali ya Jua kwa walemavu wa ngozi, ambapo wamepata pesa hizo baada ya kuuza vitabu walivyoviandika wenyewe wakiwa shule pamoja na kuuza Fulana walizozitengeneza wenyewe wakiwa Shuleni hapo. Watoto hao kutoka nchi mbalimbali wamesema kuwa Vitabu na fulana zao, nyingi wameziuza nchini   Zanzibar.

Watoto hao pia walifanikiwa kupiga picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi  Vicky Ntetema ,  na wanaonekana wakiwa katika nyuso za furaha kabisa. Ambapo Bi Nketema amewataka Watanzania kuwa na Mtizamo Chanya wa kuwasaidia Albino kwa kuiga Mfano wa watoto hao

AJALI MBAYA SANA KWA MWAKA HUU HII HAPA DUHHHHHHH

PICHA KWA HISANI YA HABARI MPASUKO

Ajali ilitokea kwenye eneo la Mboga karibu na Chalinze, millardayo.com haijapata taarifa zozote za vifo ila abiria wengi wamejeruhiwa.

.

.

.

.

.

..

.

.

.

Kondakta wa basi ndio huyu ambae aliteguka kiuno ambapo kuna mama ambae mguu wake ulikatika.

..

Leave a Comment

KAMA JANA HUKUONA BACA ALIVYOCHEZEA KICHAPO CHEKI HAPA

May 2, 2013 at 4:24 pm (Uncategorized)

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

Leave a Comment

« Older entries